Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 19

Yohana 19:23-33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
23Baada ya askari kumsulibisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo, Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.
24Kisha wakasemezana wao kwa wao, “Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani.” Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura.”
25Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
26Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!”
27Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.
28Baada ya hilo, Hali Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, “Naona kiu.”
29Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
30Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
31Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
32Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
33Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake.

Read Yohana 19Yohana 19
Compare Yohana 19:23-33Yohana 19:23-33