Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 16

Yohana 16:17-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Baadhi ya wanafunzi wake wakaambizana, “Ni nini anachotuambia, “muda mfupi, na hamtaniona tena,' na, kisha, mda mfupi mtaniona,' na, 'kwa sababu naenda kwa Baba?”
18Kwa hiyo wakasema, “Ni kitu gani anachosema, 'Bado mda mfupi'? Hatujui asemavyo.”
19Yesu aliona kuwa walitamani kumuuliza, naye akawaambia, “Mnajiuliza wenyewe kuhusu hili, nilivyosema, 'Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi mtaniona'?
20Amin, amin, nawaambia, mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utashangilia, mtakuwa na huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
21Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.
22Ninyi pia mna huzuni sasa, lakini nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi na hakuna atakayeweza kuiondoa furaha yenu.
23Siku hiyo hamtaniuliza maswali. Amin, Amin, nawaambia, Mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu.
24Mpaka sasa hamjaomba lolote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea ili kwamba furaha yenu ikamilike.
25Nimezungumza na ninyi kwa lugha isiyoeleweka, lakini saa inakuja ambapo sitazungumza kwa lugha isiyoeleweka lakini badala yake nitawaambia waziwazi kuhusu Baba.
26Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitaomba kwa Baba kwa ajili yenu;
27Kwa kuwa Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na kwa sababu mmeniamini kuwa nimetoka kwa Baba.
28Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni; tena, naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba”.
29Wanafunzi wake wakamwambia, “Unaona, sasa unaongea wazi wazi na hautumii mafumbo.

Read Yohana 16Yohana 16
Compare Yohana 16:17-29Yohana 16:17-29