Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 10

Yohana 10:3-31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwatoa nje.
4Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.
5Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawazijui sauti za wageni.”
6Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.
7Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.
8Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.
9Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.
10Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.
11Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
12Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija na huwaacha na kuwakimbia kondoo.
13Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.
14Mimi ni mchungaji mwema, na ninawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi.
15Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
16Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.
17Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.
18Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.”
19Mgawanyiko tena ukatokea kati ya wayahudi kwa sababu ya maneno haya.
20Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?”
21Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?”
22Ndipo ikaja Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.
23Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.
24Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.
25Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
26Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
27Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.
28Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.
29Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
30Mimi na Baba tu mmoja.”
31Wakabeba mawe ili wamponde tena.

Read Yohana 10Yohana 10
Compare Yohana 10:3-31Yohana 10:3-31