Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 10

Yohana 10:25-40

Help us?
Click on verse(s) to share them!
25Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.
26Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.
27Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.
28Nimewapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.
29Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.
30Mimi na Baba tu mmoja.”
31Wakabeba mawe ili wamponde tena.
32Yesu akawajibu, “Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kuniponda mawe?”
33Wayahudi wakamjibu, “Hatukupondi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu.”
34Yesu akawajibu, “Haikuandikwa katika sheria yenu, 'Nilisema, “Ninyi ni miungu”'?”
35Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),
36mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, 'Unakufuru,' kwa sababu nilisema, 'mimi ni Mwana wa Mungu'?
37“Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.
38Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba.”
39Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao.
40Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.

Read Yohana 10Yohana 10
Compare Yohana 10:25-40Yohana 10:25-40