Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wimbo wa Sulemani - Wimbo wa Sulemani 8

Wimbo wa Sulemani 8:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliye nyonya ziwa la mama yangu. Ili kwamba kila ningekuona nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.
2Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, na utanifundisha. Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine
4Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza
5Ni nani huyu anaye kuja kutoka nyikani, amemuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe.
6Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.
7Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe
8Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Nini tutamfanyia dada yetu siku hatakayo ahidiwa kuolewa?
9Kama ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
10Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
11Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao watalitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake.
12Shamba langu ka mzabibu ni langu, shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanao tunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.

Read Wimbo wa Sulemani 8Wimbo wa Sulemani 8
Compare Wimbo wa Sulemani 8:1-12Wimbo wa Sulemani 8:1-12