Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wimbo wa Sulemani - Wimbo wa Sulemani 7

Wimbo wa Sulemani 7:2-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Kitovu chako ni kama duara la bakuli; kamwe kisikose mchanganyiko wa mvinyo. Tumbo lako ni kama ngano iliyo umuka na kuzungushiwa nyinyoro.
3Maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala.
4Shingo yako ni kama mnara wa pembe; macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni kwenye lango la Bathi Rabimu. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ambao watazama Damasko.
5Kichwa chako ni kama Karmeli; nywele kichwani mwako ni za zambarau nyeusi. Mfalme amestaajabishwa na vifundo vyake vya nywele.
6Jinsi gani ulivyo mzuri na wakupendeza, mpenzi, na mazuri yako.
7Urefu wako ni wa kama mti wa mtende, na maziwa yako kama vifungu vya matunda.
8Niliwaza, “Ninataka kuupanda huo mti wa mtende; nitashika matawi yake.” Maziwa yako nayawe kama vifungu vya mizabibu, na harufu ya pua yako yawe kama mapera.
9Mdomo wako na uwe kama mvinyo bora, ukishuka taratibu kwa mpenzi wangu, ukiteleza kwenye midomo yetu na meno. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
10Mimi ni wa mpenzi wangu, na ananitamani.
11Njoo, mpenzi wangu, twende nje ya mji; tu lala usiku kwenye vijiji.
12Tuamke mapema twende kwenye mashamba ya mizabibu; tuone kama mizabibu imemea, kama imechipua, na kama mikomamanga imetoa mau. Pale nitakupa penzi langu.

Read Wimbo wa Sulemani 7Wimbo wa Sulemani 7
Compare Wimbo wa Sulemani 7:2-12Wimbo wa Sulemani 7:2-12