Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Wimbo wa Sulemani - Wimbo wa Sulemani 6

Wimbo wa Sulemani 6:4-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele.
5Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yana nizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi.
6Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja aliyefiwa.
7Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake
8Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wadogo bila idadi.
9Hua wangu, asiye na doa wangu, ni yeye pekee; ni binti muhimu wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wamalikia na masuria walimuona pia, na wakamsifu: Kile walicho sema wamalikia na masuria
10“Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, ana ng'aa kama jua, uamasisha kama bendera ya jeshi?” Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe
11Nimeenda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu imechipua, na kama mikomamanga imestawi.
12Nilikuwa nina furaha nikahisi kama nimepakia gari ya farasi la mtoto wa mfalme. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye

Read Wimbo wa Sulemani 6Wimbo wa Sulemani 6
Compare Wimbo wa Sulemani 6:4-12Wimbo wa Sulemani 6:4-12