7Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
8Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya Amana, kutoka juu ya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, kutoka mashimo ya milima ya chuwi.