Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 7

Warumi 7:17-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Lakini sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
18Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai jambo jema. Kwa kuwa tamaa ya lililo jema imo ndani yangu, lakini silitendi.
19Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi, bali lile ovu nisilolipenda ndilo nilitendalo.
20Sasa kama natenda lile nisilolipenda, si mimi binafsi nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21Nimefahama, tena, imo kanuni ndani yangu ya kutaka kutenda lililo jema, lakini uovu hakika umo ndani yangu.
22Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani.
23Lakini naona kanuni iliyo tofauti katika viungo vya mwili wangu. Inapiga vita dhidi ya kanuni mpya katika akili zangu. Inanifanya mimi mateka kwa kanuni ya dhambi iliyo katika viungo vya mwili wangu.
24Mimi ni mtu wa huzuni! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Read Warumi 7Warumi 7
Compare Warumi 7:17-24Warumi 7:17-24