Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Warumi - Warumi 6

Warumi 6:2-6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Hata kidogo! Kuhusu dhambi sisi tumekufa—tutaendeleaje kuishi tena katika dhambi?
3Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake.
4Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.
5Maana, kama sisi tumeungana naye katika kufa kama yeye, vivyo hivyo tutaungana naye kwa kufufuliwa kutoka wafu kama yeye.
6Tunajua kwamba utu wetu wa kale ulisulubiwa pamoja na Kristo, ili hali ya dhambi iharibiwe, tusiwe tena watumwa wa dhambi.

Read Warumi 6Warumi 6
Compare Warumi 6:2-6Warumi 6:2-6