Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 2

Warumi 2:3-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Lakini wewe tafakari hili, wewe ambaye unahukumu wale wanaotenda mambo hayo ingawa nawe unafanya mambo yayo hayo. Je utaepuka hukumu ya Mungu?
4Au unafikiri kidogo sana juu ya wingi wa wema wake, kuchelewa kwa adhabu yake, na uvumilivu wake? Je, hujui kwamba wema wake unapaswa kukuelekeza katika toba?
5Bali kwa kadiri ya ugumu wako na kwa moyo wako usio na toba wajiwekea mwenyewe akiba ya ghadhabu kwa siku ile ya ghadhabu, yaani, siku ile ya ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.
6Yeye atamlipa kila mtu kipimo sawa na matendo yake:
7kwa wale ambao kwa uthabiti wa matendo mema wametafuta sifa, heshima na kutokuharibika, atawapa uzima wa milele.
8Lakini kwa wale ambao ni wabinafsi, wasioitii kweli bali hutii dhuluma, ghadhabu na hasira kali itakuja.
9Mungu ataleta dhiki na shida juu ya kila nafsi ya binadamu aliyefanya uovu, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
10Lakini sifa, heshima na amani itakuja kwa kila mtu atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.
11Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.
12Kwa maana kama vile wengi waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na kama vile wengi waliokosa kulingana na sheria watahukumiwa kwa sheria.
13Maana si wasikiaji wa sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.
14Kwa maana watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanafanya kwa asili mambo ya sheria, wao, wamekuwa sheria kwa nafsi zao, ingawa wao hawana sheria.
15Kwa hili wanaonesha kwamba matendo yanayohitajika kwa mujibu wa sheria yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia zinawashuhudia wao, na mawazo yao wenyewe ama huwashitaki au huwalinda wao wenyewe
16na pia kwa Mungu. Haya yatatokea katika siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu wote, sawasawa na injili yangu, kwa njia ya Yesu Kristo.
17Tuseme kwamba unajiita mwenyewe Myahudi, aliyekaa katika sheria, shangilia kwa kujisifu katika Mungu,
18yajue mapenzi yake, na kupima mambo ambayo yanatofautiana nayo, baada ya kuagizwa na sheria.

Read Warumi 2Warumi 2
Compare Warumi 2:3-18Warumi 2:3-18