Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 2

Warumi 2:15-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
15Kwa hili wanaonesha kwamba matendo yanayohitajika kwa mujibu wa sheria yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia zinawashuhudia wao, na mawazo yao wenyewe ama huwashitaki au huwalinda wao wenyewe
16na pia kwa Mungu. Haya yatatokea katika siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu wote, sawasawa na injili yangu, kwa njia ya Yesu Kristo.
17Tuseme kwamba unajiita mwenyewe Myahudi, aliyekaa katika sheria, shangilia kwa kujisifu katika Mungu,
18yajue mapenzi yake, na kupima mambo ambayo yanatofautiana nayo, baada ya kuagizwa na sheria.
19Na tuseme kwamba una ujasiri kwamba wewe mwenyewe ni kiongozi wa kipofu, mwanga kwa wale walio gizani,
20msahihishaji wa wajinga, mwalimu wa watoto, na kwamba unayo katika sheria jinsi ya elimu na kweli.
21Wewe basi, uhubiriye mwingine, je, hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kutokuiba, je wewe huiba?
22Wewe usemae usizini, je unazini? Wewe uchukiaye sanamu, je unaiba hekaluni?
23Wewe ujisifuye katika sheria, je haumfedheheshi Mungu katika kuvunja sheria?
24Kwa maana “jina la Mungu linafedheheshwa kati ya watu wa mataifa kwa sababu yenu,” kama ilivyoandikwa.
25Kwa maana Kutahiriwa kweli kwafaa kama ukitii sheria, lakini kama wewe ni mkiukaji wa sheria, kutahiriwa kwako kunakuwa kutokutahiriwa.
26Basi, ikiwa, mtu asiyetahiriwa anaendelea kushika matakwa ya sheria, je kutokutahiriwa kwake hakutachukuliwa kana kwamba ametahiriwa?

Read Warumi 2Warumi 2
Compare Warumi 2:15-26Warumi 2:15-26