Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Warumi - Warumi 15

Warumi 15:7-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Basi, karibishaneni kwa ajili ya utukufu wa Mungu kama naye Kristo alivyowakaribisheni.
8Maana, nawaambieni Kristo aliwatumikia Wayahudi apate kuonyesha uaminifu wa Mungu, na zile ahadi Mungu alizowapa babu zetu zipate kutimia;
9ili nao watu wa mataifa mengine wapate kumtukuza Mungu kwa sababu ya huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Kwa sababu hiyo, nitakusifu miongoni mwa watu wa mataifa. Nitaziimba sifa za jina lako.”
10Tena Maandiko yasema: “Furahini, enyi watu wa mataifa; furahini pamoja na watu wake.”
11Na tena: “Enyi mataifa yote, msifuni Bwana; enyi watu wote, msifuni.”
12Tena Isaya asema: “Atatokea mtu katika ukoo wa Yese, naye atawatawala watu wa mataifa; nao watamtumainia.”
13Basi, Mungu aliye msingi wa matumaini, awajazeni furaha yote na amani kutokana na imani yenu; tumaini lenu lipate kuongezeka kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Read Warumi 15Warumi 15
Compare Warumi 15:7-13Warumi 15:7-13