Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 14

Warumi 14:10-20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Lakini wewe, kwa nini unamuhukumu ndugu yako? Na wewe, kwa nini unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
11Kwa kuwa imeandikwa, “Kama niishivyo,” asema Bwana, “Kwangu mimi kila goti litapigwa, na kila ulimi utatoa sifa kwa Mungu.”
12Hivyo basi, kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu.
13Kwa hiyo, tusiendelee tena kuhukumiana, lakini badala yake amua hivi, kwamba hakuna atakaye weka kikwazo au mtego kwa ndugu yake.
14Ninajua na nimeshawishika katika Bwana Yesu, kwamba hakuna kitu kilicho najisi chenyewe. Ni kwa yeye tu anayedhani kuwa chochote ni najisi, kwa kuwa kwake ni najisi.
15Ikiwa kwa sababu ya chakula ndugu yako anahuzunika, hautembei tena katika upendo. Usimharibu kwa chakula chako mtu ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa.
16Hivyo msiruhusu matendo yenu mema yakasababisha watu kuwadhihaki.
17Kwa kuwa ufalme wa Mungu si kwa ajili ya chakula na kinywaji, bali ni kwa ajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu.
18Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo kwa jinsi hii amekubalika kwa Mungu na amekubalika kwa watu.
19Kwa hiyo basi, na tufuate mambo ya amani na mambo ambayo humjenga mtu na mwingine.
20Usiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya chakula. Vitu vyote kwa kweli ni safi, lakini ni vibaya kwa mtu yule ambaye hula na kumsababisha yeye kujikwaa.

Read Warumi 14Warumi 14
Compare Warumi 14:10-20Warumi 14:10-20