Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Warumi - Warumi 10

Warumi 10:15-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
15Na jinsi gani wanaweza kuhubiri, isipokuwa wametumwa? - Kama ilivyoandikwa, “Jinsi gani ni mizuri miguu ya wale ambao wanatangaza habari za furaha za mambo mema!”
16Lakini wote hawakusikiliza injili. Kwa kuwa Isaya hunena, “Bwana, ni nani aliyesikia ujumbe wetu?”
17Hivyo imani huja kutokana na kusikia, na kusikia kwa neno la Kristo.
18Lakini nasema, “Je hawakusikia?” Ndiyo, kwa hakika sana. “Sauti yao imekwisha toka nje katika nchi yote, na maneno yao kwenda miisho ya dunia.”
19Zaidi ya yote, Ninasema, “Je Israel hakujua?” Kwanza Musa hunena, “Nitawachokoza kuwatia wivu kwa watu ambao si taifa. Kwa njia ya taifa lisilo na uelewa, nitawachochea hadi mkasirike.”
20Na Isaya ni jasiri sana na husema, “Nilipatikana na wale ambao hawakunitafuta. Nilionekana kwa wale ambao hawakunihitaji.”
21Lakini kwa Israel husema, “Siku zote nilinyoosha mikono yangu kwa wasiotii na kwa watu wagumu.”

Read Warumi 10Warumi 10
Compare Warumi 10:15-21Warumi 10:15-21