Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Warumi - Warumi 10

Warumi 10:11-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Maandiko Matakatifu yasema: “Kila amwaminiye hatakuwa na sababu ya kuaibika.”
12Jambo hili ni kwa wote, kwani hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi; Bwana wa wote ni mmoja, naye ni mkarimu sana kwao wote wamwombao.
13Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.”
14Basi, watamwombaje yeye ambaye hawamwamini? Tena, watamwaminije kama hawajapata kusikia habari zake? Na watasikiaje habari zake kama hakuna mhubiri?
15Na watu watahubirije kama hawakutumwa? Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Ni jambo la kupendeza mno kuja kwa wale wanaohubiri Habari Njema!”
16Lakini wote hawakuipokea hiyo Habari Njema. Maana Isaya alisema: “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?”
17Hivyo basi, imani inatokana na kuusikiliza ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.
18Lakini nauliza: je, hawakuusikia huo ujumbe? Naam, waliusikia; kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Sauti yao imeenea duniani kote; maneno yao yamefika mpaka kingo za ulimwengu.”
19Tena nauliza: je, yawezekana kwamba watu wa Israeli hawakufahamu? Mose mwenyewe ni kwa kwanza kujibu: “Nitawafanyeni mwaonee wivu watu ambao si taifa; nitawafanyeni muwe na hasira juu ya taifa la watu wapumbavu.”
20Tena Isaya anathubutu hata kusema: “Wale ambao hawakunitafuta wamenipata; nimejionyesha kwao wasiouliza habari zangu.”
21Lakini kuhusu Israeli anasema: “Mchana kutwa niliwanyoshea mikono yangu watu waasi na wasiotii.”

Read Warumi 10Warumi 10
Compare Warumi 10:11-21Warumi 10:11-21