Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Waamuzi - Waamuzi 6

Waamuzi 6:21-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
21Kisha malaika wa Bwana akashika ncha ya fimbo mkononi mwake. Kwa hiyo akagusa nyama na mikate isiyotiwa chachu; moto ukatoka nje ya mwamba, ukateketeza nyama na mikate isiyotiwa chachu. Kisha malaika wa Bwana akaenda, na Gideoni hakuweza kumwona tena.
22Gideoni alielewa kuwa yule alikuwa malaika wa Bwana. Gideoni akasema, “Ewe Bwana MUNGU! Kwa maana nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!”
23Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope, huwezi kufa.”
24Basi Gideoni akamjengea Bwana madhabahu huko. Aliiita, “Bwana ni Amani.” Hadi leo bado iko katika Ofra ya jamaa ya Waabiezeri.

Read Waamuzi 6Waamuzi 6
Compare Waamuzi 6:21-24Waamuzi 6:21-24