Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ruth

Ruth 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Basi Elimeleki mme wa Naomi, alikuwa na jamaa aitwaye Boazi, aliye kuwa tajiri, na mtu maarufu.
2Ruth, Mmoabu, alimwambia Naomi, “Ngoja niende nikakusanye mabaki ya chakula katika shamba. Nitamfuata yeyote ambaye nitapata kibali machoni pake.” Hivyo naomi akamwambia, “Nenda, mwanangu.”
3Ruth alienda kuvuna kwenye shamba akiwafuata kwa nyuma wavunaji. Na kumbe ile sehemu ya shamba ilikuwa ni mali ya Boazi, aliyekuwa na mahusiano na Elimeleki.
4Tazama, Boazi alikuja kutoka bethelehemu na kuwaambia wavunaji, “Yahweh awe nanyi.” Wakamjibu, “Yahweh akubariki.”
5Ndipo Boazi akamwambia mtumishi wake aliyekuwa akiwasimamia wavunaji, “Vipi bwana huyu msichana ni wa nani?”
6Mtumishi msimamizi wa wavunaji alijibu na kusema, “Ni msichana Mmoabu aliyerudi na Naomi kutoka nchi ya Moabu.
7Aliniambia, 'Tafadhali niruhusu kuvuna na kukusanya mabaki ya wavunaji.' Hivyo alikuja na ameendelea kuvuna toka asubuhi mpaka sasa, isipokuwa amepumzika kidogo katika nyumba.”
8Kisha Boazi akamwambia Ruth, “Unanisikiliza, mwanangu? Usiende kuvuna kwenye shamba lingine; usiondoke shambani kwangu. Badala yake, baki hapa na wasichana wangu wa kazi.
9Yaelekeze tu macho yako kwenye shamba ambamo wanaume wanavuna na ufuatie nyuma ya wanawake wengine. Je, sikuwaelekeza wanaume wasikuguse? Na upatapo kiu, unaweza kwenda kunywa maji kwenye mtungi ambao wanaume wamejaza.”
10Ndipo akapiga magoti mbele ya Boazi, na kugusisha kichwa chake chini. Akamwambia, “Kwa nini nimepata kibali machoni pako, hata unijali mimi mgeni?”
11Boazi akajibu na kumwabia, “Nimekwisha ambiwa, yote uliyo yafanya tangu mme wako afariki. Umewaacha baba yako, mama, na nchi uliyozaliwa kumfuata mama mkwe wako na kuja kwa watu usiowajua.
12Yahweh akulipe kwa matendo yako. Yahweh akulipe kwa wingi, Mungu wa Israeli, ambaye chini ya mbawa zake umepata kimbilio.”
13Ruth akasema, “Nipate kibali machoni pako, bwana wangu, kwa kuwa umenifariji, na umeongea wema kwangu, ingawa mimi sio mmoja wa watumishi wako wa kike.”
14Wakati wa chakula Boazi alimwambia Ruth, “Njoo hapa, ule baadhi ya mikate, na uchovye kipande katika divai.” Alikaa kando ya wavunaji, na Boazi akampatia kiasi cha nafaka zilizo kaangwa. Ruth alikula mpaka alipotosheka na kusaza.
15Alipoinuka kwenda kuvuna, Boazi aliamuru vijana wake, akisema, “Mwacheni avune hata katika masuke, na msimwambie lolote baya.
16Na pia muachie baadhi ya masuke katika vifurushi kwa ajili yake, na muaache ili ayavune. Msimkemee.”
17Kwa hiyo alivuna mpaka jioni. Kisha akatenganisha nafaka na majani ambayo amevuna, nazo nafaka zilikuwa kama efa moja ya shairi.
18Akazibeba na kwenda katika mji. Ndipo mama mkwe wake aliona kile alichokivuna. Ruth pia alimletea mama mkwe wake nafaka zilizo kaangwa alizobakiza kwenye chakula chake.

19Mama mkwe wake akamwambia, “Umevunia wapi uliko vunia leo? Ulienda kufanyia wapi kazi? abarikiwe mtu aliye kusaidia.” Ndipo Ruth akamwambia mama mkwe wake kuhusu mtu aliye miliki shamba alilokuwa akifanya kazi. Alimwambia, “Jina la mtu ambaye alimiliki shamba nililokuwa nikifanya kazi ni Boazi.”
20Naomi akamwambia Ruth, “Abarikiwe na Yahweh, ambaye hakuondoa uaminifu wake kwa walio hai na wafu.” Naomi akamwambia, “Huyo mtu ni jamaa wa karibu nasi, ni jamaa yetu mkombozi.”
21Ruth Mmoabu akamwambia, “Ni kweli, aliniambia, 'Ukae karibu na vijana wangu wa kiume mpaka watakapo maliza mavuno yangu yote.'”
22Naomi akamwambia Ruth mke wa mtoto wake wa kiume, “Ni vizuri, mwanangu, kuwa uende pamoja na wasichana wake wa kazi, ili kwamba usije pata madhara yeyote katika shamba lolote.”
23Kwa hiyo alikaa karibu na wafanyakazi wa kike ili avune mpaka mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano. Na alikuwa akiishi pamoja na mama mkwe wake.