Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Torati

Torati 15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kila mwisho wa kila miaka saba, mnapaswa kufuta madeni.
2Hii ni tabia ya ukombozi. Kila mkopeshaji atafuta kile alichompa jirani yake, hata dai kutoka kwa jirani yake au ndugu yake kwa sababu ufutaji wa madeni wa Yahwe umetangazwa.
3Kutoka kwa mgeni mnaweza kudai; lakini kwa chochote chenu kilicho na ndugu yenu mnapaswa mkitoe.
4Hata hivyo, pasiwepo maskini miongoni mwenu (kwa kuwa Yahwe kwa hakika atawabariki kwenye nchi ambayo anawapa kama urithi kumiliki)
5kama peke yenu mnasikiliza kwa bidii sauti ya Yahwe Mungu wenu, kuzishika amri zote ambazo anawaamuru leo.
6Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu atawabariki, kama alivyowaahidia; mtakopesha mataifa mengi, lakini hamtaazima; mtaongoza juu ya mataifa mengi, lakini hayatawaongoza ninyi.
7Kama kuna mtu maskini miongoni mwenu, moja wa ndugu zenu, ndani ya malango yenu yoyote kwenye nchi yenu ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, msifanye migumu mioyo yenu wala kufunga mkono wenu toka kwa ndugu yenu,
8Lakini mnapaswa hakika kufungua mkono wenu kwake na hakika mkopeshe yeye vya kutosha hitaji lake.
9Muwe makini kutokuwa na wazo ovu au potovu katika moyo wenu, kusema, “Mwaka wa saba, mwaka wa ukombozi u karibu; ili kwamba msiwe wachoyo kuhusiana na ndugu zenu maskini na haumpi chochote; anaweza kumlilia Yahwe kuhusu nyie, na itakuwa dhambi yenu.
10Mnapaswa kwa hakika mmpe, na moyo wenu hampaswi kuhuzunika wakati mnampa, kwa sababu kurudishiwa kwa Yahwe huyu Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika chochote mnaweka mkono wenu.
11Kwa kuwa maskini kamwe hatakoma kuishi katika nchi, kwa hiyo nakuamuru wewe na kusema, “Unapaswa kwa hakika ufungue mkono wako kwa ndugu yako, kwa mhitaji wako, na kwa maskini wako katika nchi yako.
12Kama ndugu yako, ni mwebrania wa kiume au mwebrania wa kike, ameuzwa kwako na anakutumikia kwa miaka saba, basi katika mwaka wa saba unapaswa umwache aende zake huru.
13Unapomwacha aende zake huru, usimwache aende mkono mtupu.
14Unapaswa kwa ukarimu hutoe kwake kutoka mifugo yako, kutoka pura iliyo chini, na kinu chako cha mvinyo. Kama Yahwe Mungu wako alivyokubariki, unapaswa umpe yeye.
15Unapaswa kukumbuka kwamba ulikuwa mtumwa kwenye nchi ya Misri, na kwamba Yahwe Mungu wako alikukomboa; kwa hiyo ninakuamuru leo kufanya hivi.
16Itakuwa kwamba kama atasema kwako, “Sitaenda mbali yako; kwa sababu anakupenda na nyumba yako, na kwa sababu ni mzuri kwako,
17basi unapaswa kuchukua uma na msukumo kupitia sikio lake kwenye mlango, na atakuwa mtumwa wako milele. Na pia kwa mtumwa wako wa kike utafanya vilevile.
18Isionekane kuwa vigumu kwako kumwachia aende zake huru, kwa sababu amekutumikia kwa miaka sita na amekupa mara mbili udhamani wa mtu aliyeajiriwa. Yahwe Mungu wako atakubariki katika yote unayofanya.

19Wazao wote wa kwanza wa kiume katika wanyama na mifugo wako unapaswa uwatenge kwa Yahwe Mungu wako. Hautafanya kazi na mzao wa kwanza wa wanyama wako wala kumnyoa mzao wa kwanza wa mfugo wako.
20Unapaswa umle mzaliwa wa kwanza mbele ya Yahwe Mungu wako kila mwaka katika eneo ambalo Yahwe atachagua, wewe na nyumba yako.
21Kama ina kasoro yoyote- kwa mfano, kama ni kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote- haupaswi kumtoa dhabihu kwa Yahwe Mungu wako.
22Utamla ndani ya malango yako; mtu asiye najisi na aliye najisi ni sawa unapaswa kula, kama ungekula paa au kulungu.
23Pekee haupaswi kunywa damu yake; unapaswa kuimwanga damu yake juu ya ardhi kama maji.