Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana

Yohana 11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Alitokea Bethania, kijiji cha Mariamu na dada yake Martha.
2Alikuwa ni Mariamu yule yule aliyempaka Bwana Marhamu na kumfuta miguu yake kwa nywele zake, ambaye ndugu yake Lazaro alikuwa ni mgonjwa.
3Ndipo dada hawa walituma ujumbe kwa Yesu na kusema, “Bwana, angalia yule umpendaye anaumwa.”
4Yesu aliposikia alisema, “Ugonjwa huu si wa mauti, lakini, badala yake ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika huo Ugonjwa.”
5Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.
6Aliposikia kuwa Lazaro ni mgonjwa, Yesu alikaa siku mbili zaidi mahali alipokuwa.
7Ndipo baada ya hili aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni Uyahudi tena.”
8Wanafunzi wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wakijaribu kukuponda mawe, na wewe unataka kurudi huko tena?”
9Yesu akawajibu, “Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa nuru ya mchana.
10Hata hivyo, ikiwa atatembea usiku, atajikwaa kwa sababu nuru haiko ndani yake.”
11Yesu akasema mambo haya, na baada ya mambo haya, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini ninakwenda ili kwamba nipate kumuamsha kutoka usingizini.”
12Ndipo wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala, ataamka.
13Wakati huu Yesu alikuwa akizungumza habari za kifo cha Lazaro, lakini wao walidhani anazungumza juu ya kulala usingizi.
14Ndipo Yesu akazungumza nao wazi wazi, “Lazaro amekufa.
15Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo kule ili kwamba mpate kuamini. Twendeni kwake.”
16Basi Tomaso, aliyeitwa Pacha, aliwaambia wanafunzi wenzake, “Nasi twendeni pia tukafe pamoja na Yesu.”
17Wakati Yesu alipokuja, alikuta kwamba Lazaro tayari amekwishakuwa kaburini siku nne.
18Nayo Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kama kilomita arobaini na tano hivi.

19Wengi kati ya Wayahudi wakaja kwa Martha na Mariamu kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.
20Ndipo Martha aliposikia kuwa Yesu anakuja, alienda kukutana naye, lakini Mariamu aliendelea kukaa nyumbani.
21Ndipo Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa.
22Hata sasa, najua ya kuwa lolote utakaloomba kutoka kwa Mungu, atakupatia.”
23Yesu akamwambia, kaka yako atafufuka tena.”
24Martha akamwambia, najua kwamba atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.”
25Yesu akamwambia, “Mimi ni ufufuo na uzima; yeye aniaminiye, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi;
26na yeye aishiye na kuniamini mimi hatakufa. Unaamini hili?”
27Akamwambia, “Ndiyo, Bwana naamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye katika ulimwengu.”
28Alipokwisha kusema hili, alienda zake na kumwita dada yake Mariamu faraghani. Akasema, “Mwalimu yuko hapa na anakuita.”
29Mariamu aliposikia haya, aliinuka kwa haraka na kwenda kwa Yesu.
30Naye Yesu alikuwa hajaja bado ndani ya kijiji, bali alikuwa bado mahali alipokutana na Martha.
31Ndipo Wayahudi waliokuwa na Mariamu katika nyumba na wale waliokuwa wakimfariji, walipomuona akiinuka haraka na kutoka nje, walimfuata; walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko.
32Ndipo Mariamu, alipofika pale Yesu alipokuwa alimuona na, alianguka chini ya miguu yake na kumwambia, “Bwana, kama ungelikuwa hapa, ndugu yangu asingelikufa.”
33Yesu alipomuona analia, na Wayahudi waliokuja pamoja naye walikuwa wakilia pia, aliomboleza katika roho na kufadhaika;
34akasema, “Mmemlaza wapi? wakamwambia, Bwana, njoo utazame.”
35Yesu akalia.
36Ndipo Wayahudi wakasema, “Angalia alivyompenda Lazaro!”

37Lakini wengine kati yao wakasema, “Siyo huyu, mtu aliyeyafumbua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya huyu mtu asife?”
38Ndipo Yesu, hali akiomboleza nafsini mwake tena, alienda kwenye kaburi. Sasa lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39Yesu akasema, “Liondoweni jiwe.” Martha, dada yake na Lazaro, yeye aliyekufa, akamwambia Yesu, “Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne.”
40Yesu akamwambia, “Mimi sikukuwaambia ya kwamba, kama ukiamini, utauona utukufu wa Mungu?”
41Kwa hiyo wakaliondoa jiwe. Yesu akainua macho yake juu na kusema, “Baba, nakushukuru kwa kuwa unanisikiliza.
42Nilijua kwamba unanisikia mara zote, lakini ni kwa sababu ya kusanyiko ambalo limesimama kunizunguka kwamba nimesema haya, ili kwamba wapate kuamini kuwa wewe umenituma.”
43Baada ya kusema haya, alilia kwa sauti kubwa, “Lazaro, toka nje!”
44Mfu alitoka nje amefungwa mikono na miguu kwa sanda za kuzikia, na uso wake ulifungwa na kitambaa.” Yesu akawaambia, “Mfungueni mkamwache aende.”
45Ndipo Wayahudi wengi waliokuja kwa Mariamu na kuona Yesu alichofanya, walimwamini;
46lakini baadhi yao walienda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo aliyoyafanya Yesu.
47Ndipo wakuu wa Makuhani na Mafarisayo wakakusanyika pamoja katika baraza na kusema, “Tutafanya nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi.
48Ikiwa tutamwacha hivi peke yake, wote watamwamini; Warumi watakuja na kuchukua vyote mahali petu na taifa letu.”
49Hata hivyo, mtu mmoja kati yao, Kayafa, aliyekuwa kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, “Hamjui chochote kabisa.
50Hamfikirii kwamba yafaa kwa ajili yenu kwamba mtu mmoja yapasa kufa kwa ajili ya watu kuliko taifa lote kuangamia.”
51Haya hakuyasema kwa sababu yake mwenyewe, badala yake, kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule, alitabiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa;
52na si kwa taifa peke yake, bali Yesu apate vile vile kuwakusanya watoto wa Mungu ambao wametawanyika sehemu mbali mbali.
53Kwa hiyo kuanzia siku hiyo na kuendelea wakapanga namna ya kumwua Yesu.
54Yesu hakutembea tena wazi wazi kati ya Wayahudi, bali aliondoka hapo na kwenda nchi iliyo karibu na jangwa katika mji uitwao Efraimu. Hapo alikaa na wanafunzi.

55Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu, na wengi wakapanda kwenda Yerusalemu nje ya mji kabla ya Pasaka ili wapate kujitakasa wenyewe.
56Walikuwa wakimtafuta Yesu, na kuzungumza kila mmoja walipokuwa wamesimama hekaluni, “Mnafikiri nini? Kwamba hatakuja katika sikukuu?”
57Wakati huu wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba ikiwa mmoja atajua Yesu alipo, anapaswa kutoa taarifa ili kwamba wapate kumkamata.