Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka

Luka 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikawa siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri injili, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walimwendea pamoja na wazee.
2Walizungumza, wakimwambia, 'Tuambie ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Au ni nani huyo ambaye amekupa mamlaka haya?
3“Naye akajibu, akawaambia, 'Nami pia nitawauliza swali. Niambieni
4ubatizo wa Yohana. Je, ulitoka mbinguni ama kwa watu?'
5Lakini wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, 'Tukisema, `litoka mbinguni, atatuuliza,` Basi, mbona hamkumwamini?'
6Na tukisema; ilitoka kwa wanadamu; watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.'
7Basi, wakamjibu ya kwamba hawakujua ilikotoka.
8Yesu akawaambia, '“Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”
9Aliwaambia watu mfano huu, “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu.
10Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu.
11Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu.
12Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje.
13Hivyo bwana wa shamba akasema, 'Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu.'
14Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, `Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu.'
15Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?
16Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine”. 'Nao waliposikia hayo, wakasema, 'Mungu amekataa'
17Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? 'Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni'?
18Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda.'

19Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.
20Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.
21Nao wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
22Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
23Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,
24“Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, '“Ya Kaisari.”
25Naye akawaambia, 'Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.'
26Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.
27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,
28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.
29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,
30na wa pili pia.
31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.
32Baadaye yule mwanamke pia akafa.
33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.'
34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.
35Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi.
36Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.

37Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
38Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake.
39“Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema.'
40Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.
41Yesu akawaambia, “Ki vipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
43mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.'
44Daudi anamwita Kristo 'Bwana', basi atakuwaje mwana wa Daudi?”
45Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,
46'Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na wapenda salamu maalum sokoni na viti vya heshima katika masinagogi, na maeneo ya heshima karamuni.
47Wao pia hula nyumba za wajane, na wanajifanya wanasali sala ndefu. Hawa watapokea hukumu kubwa zaidi.'