Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Hesabu

Hesabu 34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1BWANA akanena na Musa akasema,
2“Waamuru watu wa Israeli na uwaambie, 'Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, nchi ambayo itakuwa mali yenu, nchi ya Kanaani na mipaka yake, mpaka wenu wa kusini utaendelea kutoka nyika ya Sini hadi mpaka wa Edomu.
3Mwisho wa mpaka wa kusini utakuwa mwisho wa bahari ya chumvi kuelekea mashariki.
4Mpaka wenu utageukia kusini kutoka mlima kuelekea Akrabimu na kupitia nyika ya Sini. na kutokea huko utaelelkea kusini mwa Kadeshi Barinea na kuelekea Hazari Adari mpaka Azimoni.
5Kutoka huko, mpaka utageuka kutoka Azimoni kuelekea kijito cha Misri na kukifuata mpaka baharini.
6Mpaka wa Magharibi utakuwa pwani ya bahari kuu. Huu ndio utakuwa mpaka wenuwa Magharibi.
7Mpaka wenu wa kaskazini utaanzia kwenye bahari kuu hadi Mlima Hori,
8kisha kutoka Mlima Hori hadi Lebo Hamathi, kisha Zedadi.
9Mpaka utaendelea hadi Zifroni na kuishia Hazari Enani. Huu ndio utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
10Kisha mtaweka alama za mpaka wenu wa mashariki ambao utaanzia Hazari Enani kuelekea kusini Shefamu.
11Kisha mpaka wa kusini utaendelea kutoka Shefamu hadi Ribla, upande wa masharikia mwa Aini. Mpaka utaedelea upande huo wa mashariki hadi upande wa mashariki wa bahari ya Kinerethi.
12Kisha mpaka utaendelea kuelekea kusini hadi mto Yorodani na hadi bahari ya chumvi. Hii ndiyo itakuwa nchi yenu, kwa kuifuata mipaka yake yote inayozunguka.'”
13Kisha Musa akawaamuru watu wa Israeli akasema, “Hii ndiyo nchi ambayo mtaipokes kwa kura, ambayo BWANA ameamuru kuwapa wale makabila tisa na nusu.
14Kabila ya uzao wa Reubeni, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na uzao wa kabila la Gadi, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na nusu ya Manase wamepata ardhi yao.
15Wale makabila mawili na nusu wameshapata mgawo wao ng'ambo ya mto Yorodani upande wa mashariki, kuelekea kule linakotokea jua.”
16BWANA akanena na Musa akasema,
17“Haya ndiyo majinaya watu watakaoigawa ardhi kwa ajili ya urithi wao: Eliazari kuhani na Joshua mwana wa Nuni.
18Mtachagua kiongozi mmoja toka kila kabila ili kuigawa ardhi kwa koo zao.

19Haya ndiyo majina ya wanaume: Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
20Kutoka kwenye kabila la uzao wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21Kutoka kabila la Benjamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
22Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Dani, Buki mwana wa Jogili.
23Kiongozi kutoka uzao wa Yusufu, kwenye kabila la Manase, Hannieli mwana wa Efodi.
24Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Efraimu, Kemueli mwana wa Shiftani.
25Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Zabuloni, Elizafani mwana wa Parinaki.
26Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Isakari, Palitieli mwana wa Azzani.
27Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi.
28Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.”
29BWANA aliwaamuru wanaume hawa kuigawa nchi ya Kanaani na kuwapa kila kabla sehemu yao.