Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1“Tena wewe, chukua maombolezo juu ya viongozi wa Israeli
2na sema, 'Mama yako alikuwa nani? Simba jike mmoja, aliishi na mtoto wa simba dume; katikati ya simba wadogo, aliwalisha watoto wake.
3Alimlea mmoja wa wale watoto kurarua wanyama wengine, na kisha alijifunza jinsi ya kuwinda watu na kuwala.
4Kisha mataifa wakasikia kuhusu yeye. Akakamatwa kwenye mtego wao, na wakamleta kwa kulabu hata nchi ya Misri.
5Kisha alipoona kwamba ingawa alikuwa akimsubiri arudi, matumaini yake sasa yalienda, hivyo alimchukua mtoto wake wengine katika watoto wake na kumlea hata kuwa mwana simba.
6Huyu mwana simba alitembea huku na huku katikati ya simba. Akawa mwana simba na kujifunza kuwinda mawindo; akala watu.
7Akawakamata wajane na kuiharibu miji. Nchi na viijazavyo vilitelekezwa kwa sababu ya sauti ya kunguruma kwake.
8Lakini mataifa yakaja juu yake kutoka mikoa yote; wakatengeneza nyavu juu yake. Akakamatwa kwenye mtego wao.
9Kwa kulabu wakamuweka kwenye tundu na kisha wakamleta hata kwa mfalme wa Babeli. Wakamleta hata kwenye ngome imara ili kwamba sauti yake isiweze kusikika juu ya milima ya Israeli.
10Mama yako alikuwa kama mzabibu uliopandwa kwenye damu yako karibu na maji. ulizaa matunda na kujaa matawi kwa sababu ya wingi wa maji.
11Ulikuwa na matawi imara yaliyokuwa yakitumika kwa ajili ya fimbo ya utawala, na kipimo chake kiliinuka juu ya matawi, na kina wake ulionekana kwa ukubwa wa majani yake.
12Lakini mzabibu uling'olewa kwa ghadhabu na kutupwa chini hata aridhini, na upepo wa mashariki uliuvunja na kunyauka na moto ukavila.
13Hivyo sasa, umepandwa jangwani, kwenye nchi ya ukame na kavu.
14Kwa kuwa moto ulitoka kwenye matawi makubwa na kuyala matunda yake. Hakuna tawi imara juu yake, hakuna fimbo ya kifalme kutawala.' Haya ni maombolezo na yataimbwa kama maombolezo.”