Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Kutoka

Kutoka 25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh akamwambia Musa,
2“Waambie Waisraeli wanitolee sadaka kila mtu nawe utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu. Lazima upokee hizi sadaka kwa ajili yangu.
3Hizi ndio sadaka utakazopokea kwao; dhahabu, fedha na shaba,
4buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na manyoya ya mbuzi;
5na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, miti ya mjohoro,
6mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;
7mawe ya shohamu na mawe mengine ya kutiwa kwa ile naivera na kwa kile kifuko cha kifuani.
8Waache wanifanyie patakatifu ili nipate kukaa kati yao.
9Lazima ufanye sawa na haya yote nikuoneshayo mfano wa maskani, na vifaa vyake, ndivyo utakavyovifanya.
10Wana paswa wafanye sanduku la mti wa mjohoro. Urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu; na upana wake moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
11Lazima ulifunike nadni kwa dhahabu safi, na utie na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
12Nawe uta yayusha katika viduara vinne vya dhahabu, na kuviweka katika miguu yake minne; viduara viwili upande mmoja, na viduara viwili upande wake wa pili.
13Nawe lazima ufanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu.
14Nawe lazima uweka hiyo miti katika vile viduara vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.
15Hiyo miti itakaa katika vile viduara vya sanduku; haitaondolewa.
16Kisha weka ndani ya sanduku hizo amri nitakazokupa.
17Nawe lazima utengeneze kifuniko cha dhahabu safi. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu.
18Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu katika hiyo miisho miwili ya kiti cha rehema.

19Weka kerubi moja mwisho mmoja wa kiti cha rehema, na kerubi la pili mwisho wa pili. Lazima hao makerubi wawe kitu kimoja na kiti cha rehema.
20Na hao makerubi watainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao. Nyuso zao makerubi zitaelekeana na zitaelekea kiti cha rehema.
21Lazima uweke kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha uwe hizo amri nitakazokupa ndani ya sanduku.
22Nami nitaonana nawe hapo katika sanduku. Nitazungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema. Itakuwa katikati ya hao makerubi mawili waliyo juu ya sanduku la ushuhuda nitakapo zungumza na wewe katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.
23Nawe fanya meza ya mti wa mshiti. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.
24Uifunike dhahabu safi na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote.
25Lazima ufanyie fremu ya kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, ukingo wa dhahabu wa kuuzunguka fremu pande zote.
26Uifanyie viduara vinne vya dhahabu na kuvitia vile viduara katika pembe zake nne, katika miguu yake minne ilipo kuwa.
27Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza.
28Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.
29Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia. Vifanye vyote vya dhahabu safi.
30Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.
31Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho.
32Nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake - matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili.
33Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara.
34Katika hicho kinara, lazima kuwe na vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake.
35Lazima kuwe na tovu chini ya matawi - mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara.
36Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho, kiwe chote pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.

37Lazima nawe uzifanye hivyo vinara saba na taa zake saba, nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.
38Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.
39Tumia talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.
40Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.