Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Kutoka

Kutoka 21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa hizi ni amri utakazoweka kabla yao:
2'kama mtanunua mtumishi wa kiebrania, atatumikia kwa miaka sita, na mwaka wa saba ataachiwa huru bila kilipwa chochote.
3Kama alikuja mwenyewe, ataenda huru kwa ridhaa yake;
4kama bwana wake atampa mke na kumzalia mwana na binti, mke pamoja na watoto wake watabaki mali ya bwana wake, na ataenda zake huru.
5Lakini kama mtumishi atasema waziwazi, “Nampenda bwana wangu, mke wangu, na watoto; sitaenda nje,”
6“kisha bwana wake atapaswa kumleta kwa Mungu. Bwana wake atapaswa kumleta katika mlango au katika muhimili wa mlango, na bwana wake atatoboa sikio lake na sindano. Kisha mtumishi wake atamtumikia kwa maisha yake yote.
7Kama mwanaume ata muuza binti wake kama mtumishi wa kike, ata weza kwenda huru kama watumishi wa kiume wanavyo enda.
8Kama hamridhishi bwana wake, aliye mtenga kwa ajili yake, kisha lazima amnunue tena. Hana ruhusa ya kumuuza kwa watu wengine wa kigeni. Hana ruhusa hiyo, sababu amemtendea kwa hila.
9Ikiwa bwana wake atamposa awe mke wa mwanae, atamtendea kama desturi zipasavyo sawa na binti zake.
10Ikiwa atajitwalia mke mwingine, asimpunguzie huyo chakula chake, nguo na haki zake za unyumba.
11Lakini asipofanyiwa mambo haya matatu, basi anaweza kwenda bure pasipo kutolewa mali.
12Mtu awaye yote ampigaye mtu hata akafa, inampasa mtu huyo auawe pia.
13Lakini kama hakumvizia, ila kwa bahati mbaya, basi nitamfanyia mahali pa kukimbilia.
14Lakini mtu akimwendea mwenzake kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata kama ni madhabahuni pangu, ili auawe.
15Yeyote atakaye mpiga baba au mama yake lazima auawe.
16Yeyote atakaye mteka mtu na kumuuza, au mtu amekutwa kama mali yake, huyo mtekaji lazima auawe.
17Yeyote atakaye mlaani baba au mama yake lazima auawe.
18Kama wanaume watapigana na mmoja akimpiga mwengine kwa jiwe au ngumi, na huyo mtu asife, lakini alazwe kitandani;
19kisha akapona na anaweza kutembea kwa gongo lake, yeye aliye mpiga lazima alipe muda aliye mpotezea; na lazima alipe matibabu yake yote. Lakini huyo mtu hana hatia ya mauaji.
20Kama mwanaume akimpiga mtumishi wake wa kiume au wa kike kwa gongo, na kama mtumishi huyo akifa kwa madhara ya pigo, kisha huyo mtu lazima ahadhibiwe.
21Walakini, mtumishi huyo akiishi siku moja au mbili, bwana aruhusiwi kuadhibiwa, kwa kuwa atateseka kupoteza mtumishi huyo.
22Kama wanaume wakipigana pamoja na wakamuumiza wanamke mwenye mimba na kuiharibu, lakini hakuna majeraha mengine kwake, kisha huyo mwanaume mwenye hatia lazima alipe kama mme wa mwanamke anavyo taka kwake, na kulipa kama hakimu anavyo kusudia.
23Lakini kama kuna majeraha makubwa, lazima utoe uhai kwa uhai, jicho kwa jicho,
24jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,
25kuchoma kwa kuchoma, jeraha kwa jeraha, au mkwaruzo kwa mkwaruzo.
26Kama mwanaume akipiga jicho la mtumishi wake kiume au mtumishi wake wa kike na kuliharibu, kisha lazima amuache mtumishi aende pasipo fidia ya jicho.
27Kama akitoa jino la mtumishi wake wa kiume au mtumishi wake wa kike, lazima amuache mtumishi kwenda huru kama fidia ya jino.
28Kama ng'ombe akimpiga mwanaume au mwanamke akafa, ng'ombe lazima apigwe mawe, na nyama yake hairuhusiwi kuliwa; lakini mmiliki wa ng'ombe lazima awe huru kwa hatia.
29Lakini kama ng'ombe alikuwa na tabia ya kupiga hapo awali, na mmiliki wake alionywa lakini hakumzuia, na ng'ombe ameua mwanaume au mwanamke, huyo ng'ombe lazima apigwe mawe, na mmiliki wake lazima auawe pia.
30Kama malipo ya uhai yanaitajika, lazima alipe chochote anachotakiwa kulipa.
31Kama ng'ombe amempiga mwana wa mwanaume au binti wake, mmiliki wa ng'ombe anapaswa kufanya kama masharti yanavyo mlazimu.
32Kama ng'ombe akimpiga mtumishi wa kiume au wakike, mmiliki wa ngombe lazima alipe shekeli thelathini za fedha, na ng'ombe lazima apigwe mawe.
33Kama mwanaume akifungua shimo, au kama mwanume akichimba shimo na asifunike, na ng'ombe au punda akaanguka ndani,
34mmiliki wa shimo lazima alipe madhara. Lazima atoe hela kwa mmiliki wa mnyama aliye kufa, na mnyama aliye kufa atakuwa wake.
35Kama ng'ombe wa mwanaume akimuumiza ng'ombe wa mwanume mwengine hadi kufa, kisha lazima wamuuze ng'ombe aliye hai na kugawana gharama, na pia lazima wagawane ng'ombe aliye kufa.
36Lakini kama ilijulikana kama ng'ombe alikuwa na tabia ya kupiga hapo awali, na mmiliki wake hakumfunga ndani, hakika lazima alipe ng'ombe kwa ng'ombe, na mnyama aliye kufa atakuwa wake.