Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 80

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Usikie, Mchungaji wa Israel, wewe uliye muongoza Yusufu kama kundi; wewe uketiye juu ya makerubi, utuangazie!
2Machoni pa Efraimu na Benjamini na Manase, uziinue nguvu zako; njoo na utuokoe.
3Mungu, uturejeshe sisi; uangaze uso wako juu yetu, nasi tutaokolewa.
4Yahwe Mungu wa majeshi, mpaka lini utawakasirikia watu wako wanapoomba?
5Umewalisha wa mkate wa machozi na umewapa machozi ili wanywe katika kiasi kikubwa.
6Umetufanya kitu kwa ajili ya majirani zetu kubishania, na maadui zetu hucheka kuhusu sisi kati yao.
7Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; nasi tutaokolewa.
8Wewe ulileta mzabibu kutoka Misri; ukawafukuza mataifa na ukaupanda.
9Uliisafisha ardhi kwa ajil yake; nao ulipata mzizi na kuijaza nchi.
10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, mierezi ya Mungu kwa matawi yake.
11Ilieneza matawi yake mbali kama bahari na mashina yake mpaka kwenye Mto Euphrates.
12Kwa nini umezibomoa kuta zake hata wapitao karibu huyachuma matunda yake.
13Ngurue wa msituni wanauharibu, na wanyama wa kondeni wanaula.
14Urudi, Ee Mungu wa majeshi; kutoka mbinguni utazame chini na uuangalie na kuujali huu mzabibu.
15Huu ni mzizi ambao mkono wako wa kuume umeupanda, mashina ambayo wewe uliyafanya yakue.
16Yamekatwa na kuchomwa; yameangamia kwa sababu ya kukemea kwako.
17Mkono wako na uwe juu ya mtu aliye mkono wako wa kuume, kwa mwana wa mtu uliyemfanya imara kwa ajili yako mwenyewe.
18Ndipo hatuta kuacha wewe; utuhuishe, nasi tutaliita jina lako.

19Yahwe, Mungu wa majeshi, uturejeshe sisi; utuangazie nuru ya uso wako, nasi tutaokolewa.