Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 67

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah
2ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote.
3Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
4Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
6Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
7Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.