Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Unihukumu mimi, Yahwe, kwa kuwa nimeenenda katika uadilifu; nimeamini katika Yahwe bila kusita.
2Unichunguze, Yahwe, na unijaribu; uujaribu usafi wa sehemu zangu za ndani na moyoni mwangu!
3Kwa maana uaminifu wa agano lako uko mbele ya macho yangu, na mwenendo wangu ni katika uaminifu wako.
4Mimi sichangamani na watu waovu, wala sichangamani na watu wanafiki.
5Ninachukia waovu, na siishi na waovu.
6Ninaosha mikono yangu kounesha sina hatia, na kuikaribia madhabahu yako, Yahwe,
7kuimba wimbo wa sauti ya sifa na kutoa taarifa ya matendo yako yote ya ajabu.
8Yahwe, ninaipenda nyumba ninayoishi, mahali ambapo utukufu wako unaishi!
9Usiniangamize pamoja na wenye dhambi, au maisha yangu na watu wenye kiu ya kumwaga damu,
10ambao katika mikono yao kuna njama, na ambao mkono wa kuume umejaa rushwa.
11Lakini kwangu mimi, nitaenenda katika uadilifu; uniokoe na unihurumie.
12Miguu yangu husimama sehemu salama; katika kusanyiko la watu nitambariki Yahwe!