Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 143

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ee Yahwe, usikie maombi yangu; sikia kuomba kwangu. Kwa sababu ya uaminifu wa agano lako na haki yako, unijibu!
2Usimuhukumu mtumishi wako, kwa kuwa machoni pako hamna aliye haki.
3Adui ameifuatia nafsi yangu; amenisukuma hadi chini; amenifanya niishi gizani kama wale ambao wamekwisha kufa siku nyingi zilizopita.
4Na roho yangu inazidiwa ndani yangu; moyo wangu unakata tamaa.
5Nakumbuka siku za zamani zilizopita; nayatafakari matendo yako yote; nawaza juu ya utimilifu wako.
6Nakunyoshea mikono yangu katika maombi; nafsi yangu inakuonea kiu katika nchi kavu. Selah
7Unijibu upesi, Yahwe, kwa sababu roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, vinginevyo nitakuwa kama wale waendao chini shimoni.
8Unifanye kusikia uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi, maana ninakuamini wewe. Unionyeshe njia niipasayo kutembea kwayo, kwa maana nakuinulia wewe nafsi yangu.
9Uniokoe dhidi ya adui zangu, Yahwe; nakimbilia kwako ili nijifiche.
10Unifundishe kufanya mapenzi yako, maana wewe ni Mungu wangu. Roho wako mwema na aniongoze mimi katika nchi ya unyoofu.
11Ee Yahwe, kwa ajili ya jina lako, unihifadhi hai; katika haki yako uitoe nafsi yangu taabuni.
12Katika uaminifu wa agano lako uwaondoshe maadui zangu na uwaangamize maadui wa uhai wangu, maana mimi ni mtumishi wako.