Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi

Zaburi 115

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu, bali kwa jina lako ulete heshima, kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na uaminifu wako.
2Kwa nini mataifa yalazimike kusema, “Yuko wapi Mungu wako?”
3Mungu wetu aliye mbinguni; hufanya chochote apendacho.
4Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
5Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
6zina masikio, lakini hazisikii; zina pua lakini hazinusi.
7Sanamu hizo zina mikono, lakini hazishiki; zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala haziongei kutoka viywani mwao.
8Wale wanao zitengeneza wanafanana nazo, vile vile yeyote anaye amini katika hizo.
9Israeli, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
10Nyumba ya Haruni, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
11Ninyi mnao mheshumu Yahwe, mwamini yeye; yeye ni msaada wenu na ngao yenu.
12Yahwe hutukumbuka sisi na atatubariki; ataibariki familia ya Israeli; atabariki familia ya Haruni.
13Atawabariki wale wanao muheshimu yeye, wote vijana na wazee.
14Yahwe na awaongeze ninyi zaidi na zaidi, ninyi pamoja na watoto wenu.
15Yahwe na awabariki, aliyeziumba mbingu na nchi.
16Mbingu ni za Yahwe; lakini nchi amewapa wanadamu.
17Wafu hawamsifu Yahwe, wala wote washukao chini kwenye ukimya;
18bali tutamtukuza Yahwe sasa na hata milele. Msifuni Yahwe.