Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Nimefanya patano na macho yangu; ni kwa namna gani tena napaswa kumtazama mwanamwali kwa tamaa?
2Ni sehemu gani kutoka kwa Mungu juu, na urithi gani kutoka kwake mwenye nguvu aliye juu?
3Nilikuwa nafikiri kwamba majanga ni kwa watu wasio na haki, na misiba ni kwa ajili ya watu watendao mabaya.
4Je Mungu hazioni njia zangu na kuzihesabu hatua zangu zote?
5Kama nimetembea katika udanganyifu, kama mguu wangu umeharakisha katika uongo,
6na nipimwe katika vipimo vilivyo sawa ili kwamba Mungu aujue uadilifu wangu.
7Kama hatua zangu zimegeuka kutoka katika njia sahihi, kama moyo wangu umetembea kwa kufuata macho yangu, na kama doa lolote la uchafu limeng'ang'ania katika mikono yangu,
8na kisha mimi nipande na mtu mwingine na ale; mavuno na yang'olewe katika shamba langu.
9Na kama moyo wangu umevutiwa na mwanamke mwingine, ikiwa nimelala na mke wa jirani yangu katika hali ya kusubiria katika mlango wake,
10na ndipo mke wangu na asage nafaka kwa mwanaume mwingine, na wanaume wengine na walale naye.
11Na kwa hilo litakuwa ni kosa kubwa; kwa kweli, utakuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi.
12Kwa kuwa ni moto ambao unateketeza kila kitu kwa uharibifu, na kwamba utaunguza mavuno yangu yote.
13Ikiwa nilikataa ombi la haki kutoka kwa watumishi wangu wa kiume na wa kike wakati walipohojiana nami,
14kisha nini basi ningefanya wakati Mungu anapoinuka ili kunishitaki mimi? Atakapokuja kunihukumu, nitamjibuje?
15Je yeye aliyenifanya mimi tumboni hakuwafanya wao pia? Je yeye si yeye yule aliyetuumba sisi wote katika tumbo?
16kama nimewanyima watu masikini matakwa yao, au kama nimesababisha macho ya wajane yafifie kwa kulia,
17au ikiwa kama nimekula kipande changu na sijawaruhusu wale wasio na baba kukila pia -
18kwasababu tangu ujana wangu yatima walikua pamoja nami kama kuwa na baba, nami nimemwongoza mama yake, mjane, tangu katika tumbo la mama yangu mwenyewe.

19ikiwa nimemwona yeyote akiangamia kwa kwa kukosa mavazi, au kama nimemwona mtu mhitaji akiwa hana nguo;
20ikiwa moyo wake haujanibariki kwasababu amekuwa hajatiwa joto na sufu ya kondoo zangu,
21ikiwa nimeinua juu mkono wangu kinyume na watu wasio na baba kwa kuwa niliona msaada wangu katika lango la mji, na kisha kuleta mashitaka dhidi yangu.
22Ndipo bega langu na lianguake kutoka katika sehemu yake, na mkono wangu uvunjike katika kiungo chake.
23Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu; kwasababu ya mawazo ya ukuu wake, nisingeweza kufanya mambo hayo.
24Kama ningeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, na kama ningesema kwa dhahabu safi, 'wewe unanifanya kuwa na tumaini';
25na kama nimefurahi kwasababu ya utajiri wangu ulikuwa mkubwa, kwa kuwa mkono wangu umepata mali nyingi, na kisha kuleta mashitaka dhidi yangu!
26Ikiwa nimeliona jua lilipowaka, au mwezi ukitembea katika mng'ao wake,
27na kama moyo wangu umevutwa kwa siri, ili kwamba mdomo wangu umeubusu mkono wangu katika ibada yao -
28hili nalo pia lingekuwa ni ubaya wa kuadhibiwa na waamuzi, kwa kuwa ningekuwa nimemkana Mungu aliyejuu.
29Ikiwa nimefurahia uharibifu wa yeyote ambaye ananichukia mimi, au kuwapa hongera wakati majanga yanapowapata, ndipo ulete mashitaka dhidi yangu!
30Kwa kweli sijauruhusu hata mdomo wangu kutenda dhambi kwa kuuomba uhai wake kwa laana.
31Ikiwa watu wa hema yangu hawajasema,' Nani aweza kumpata mtu ambaye hayashibishwa na chakula cha Ayubu?
32(hata mgeni hajawahi kukaa katika pembe ya mji, kwa kuwa siku zote nimefungua milango yangu kwa ajili ya wasafiri), na kama haiko hivyo, ndipo mlete mashitaka kinyume nami!
33Ikiwa, kama binadamu nimezificha dhambi zangu kwa kuficha hatia ndani ya kanzu yangu -
34kwa kuwa niliogopa kusanyiko kubwa, kwasababu ya matwezo ya familia yaliniogopesha, hivyo basi nilinyamaza kimya na sikuweza kwenda nje, basi nileteni mashitaka dhidi yangu!
35Ee, kama nilikuwa na mtu wa kunisikiliza! Ona, hii ni saini yangu; na Mwenye nguvu na anijibu! Ikiwa nilikuwa na shitaka rasmi ambalo adui yangu ameliandika!
36Hakika ningelibeba hadharani juu ya bega langu; ningeliweka juu kama taji.

37Ningemweleza hesabu ya hatua zangu; na kama mwana wa mfalme mwenye kujiamini ningepanda kwenda kwake.
38Kama nchi yangu ingelia dhidi yangu, na matuta yake yaomboleza pamoja,
39ikiwa nimekula mavuno yake bila kulipia au kama nimesababisha wamiliki wake kupoteza maisha yao,
40ndipo miiba na iote badala ya ngano na magugu badala ya shayiri.” Maneno ya Ayubu yamemalizika.