Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ayubu

Ayubu 12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2“Hakuna shaka ninyi wanadamu; Hekima mtakufa nayo.
3Lakini nina ufahamu kama vile ninyi; Mimi siyo duni kwenu. Ni dhhiri, ni nani asiyefahamu vitu hivyo kama hivi?
4Mimi ni kitu cha kuchekwa na jirani-Mimi, ni mmoja aliyemwita Mungu na ambaye alijibiwa na yeye! Mimi, ni mwenye haki na mtu asiyekuwa na hatia-Mimi sasa nimekuwa kitu cha kuchekwa.
5Katika mawazo yake mtu fulani aliye katika kufurahi, kuna kudharau kwa mashaka; hufikiri katika njia ambayo huleta mambo mabaya zaidi kwa wale ambao miguu yao inateleza.
6Hema za wezi hufanikiwa, na wale ambao humkasirisha Mungu huhisi salama; mikono yao wenyewe ni miungu wao.
7Lakini sasa waulize hao wanyama wa mwituni, na watakufundisha wewe; waulize ndege wa angani, na watakuambia wewe.
8Au iambie ardhi, na itakufundisha wewe; samaki wa baharini watakutangazia wewe.
9Ni myama yupi miongoni mwa hawa asiyefahamu kuwa mkono wa Yahwe umetenda haya?
10Katika mkono wake mna uzima wa kila kiumbe hai na pumzi ya wanadamu wote.
11Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile kaakaa lionjavyo chakula chake?
12Kwa wazee mna hekima; katika wingi wa siku mna ufahamu.
13Pamoja na Mungu mna hekima na ukuu; yeye anayo mashauri na ufahamu.
14Tazama, yeye huangusha chini, na haiwezekani kujengwa tena; kama yeye akimtia gerezani mtu yeyote, hakutakuwa tena kufunguliwa.
15Tazama, kama yeye akiyazuia maji, yanakauka; na kama akiyaachilia nje yanaitaabisha ardhi.
16Pamoja na yeye mna nguvu na hekima; watu ambao wamedanganywa na mdanganyi wote pamoja wako katika nguvu zake.
17Yeye huwaongoza washauri mbali bila kuvaa viatu katika huzuni; huwarudisha hakimu katika upumbavu.
18Yeye Huondoa minyororo ya mamlaka kutoka kwa wafalme; yeye hufunika viuno vyao kwa nguo.

19Yeye huwaongoza makuhani mbali bila kuvaa viatu na kuwapindua watu wakuu.
20Yeye huondoa hotuba ya wale waliokuwa wameaminiwa na huondoa mbali ufahamu wa wazee.
21Yeye humwaga aibu juu ya binti za wafalme na hufungua mishipi ya watu wenye nguvu.
22Yeye huweka wazi vitu vya kina kutoka katika giza na kuvileta nje kumuika vivuli mahali ambapa watu waliokufa wapo.
23Yeye huyafanya mataifa kuwa na nguvu, na pia huyaharibu; Yeye pia huyakuza mataifa, na pia yeye huyaongoza mbali kama wafungwa.
24Yeye huondoa mbali ufahamu kutoka kwa viongozi wa watu wa nchi; huwafanya wao kutangatanga msituni mahali pasipo na njia.
25Wao wanapapasa katika giza bila kuwa na mwanga; yeye huwafanya wao kuweweseka kama mtu mlevi.