Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yothamu alikuwa na umri wa mika ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yerusha; alikuwa binti Sadoki.
2Akafanya yaliyomema katika macho ya Yawe, akiufuta mfano wa baba yake, Uzia, katika mabo yote. Pia alijiepusha kuingia katika hekalu la Yahwe. Lakini watu bado walikuwa wanaenda katika njia za uovu.
3Akalijenga tena lango la juu la nyumba ya Yahwe, na juu ya kilima cha Ofeli akajenga sana.
4Vilevile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika mistu alijenga ngome na minara.
5Pia alipigana na mfalme wa watu wa Amoni na akawashinda. Katika mwaka huo huo, watu wa Amoni walimpa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, kori elfu kumi za shayiri. Watu wa Amoni wakampa hivyo hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.
6Kwa hiyo Yothamu akawa na nguvu sana kwa sababu alitembea imara mbele za Yahwe Mungu wake.
7Kwa mambo mengine kuhusu Yothamu, vita vyake vyote, na njia zake zote, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.
8Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi na sita kataika Yerusalemu.
9Yothamu akalala pamoja na babu zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Ahazi, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.