Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 1 Nyakati

1 Nyakati 13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Daudi akashuriana na wakuu wa jeshi la maelfu na mamia, na kila kiongozi.
2Daudi akasema kwa kusanyiko la Isaraeli, “Kama itakuwa vyema, na kama hii inatoka kwa Yahweh Mungu wetu, na tutume wajumbe kila sehemu kwa ndugu zetu walio baki maeneo yote ya Israeli, na kwa makuhani na Walawi walio kwenye miji yao. Waambiwe wajiunge nasi.
3Na tulete sanduku la Mungu wetu, kwa kuwa hatukutafuta mapenzi yake katika siku za Sauli.”
4Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote.
5Kwaiyo Daudi akakusanya Israeli yote, kutoka mto Shihori ulio Misri hadi Lebo Hamathi, kuleta sandaku la Mungu kutoka Kiriathi Yearimu.
6Daudi na Israeli yote walienda mpaka Baala, ambayo ni, Kiriathi Yearimu, ambao ni ya Yuda, kuleta sanduku la Mungu, ambalo linaitwa kwa jina la Yahweh, Yahweh, ambaye ameketi juu ya makerubi.
7Kwaiyo wakaketisha sanduku la Mungu juu ya chombo kipya cha matairi. Wakaleta nje ya nyumba ya Abinadabu. Uza na Ahio walikuwa wakilinda hicho chombo.
8Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote. Walikuwa wakiimba na vyombo vya uzi, vinubi, upatu, na tarumbeta.
9Walipo kuja eneo la kupeta mazao huko Kidoni, Uza alinyoosha mkono wake kuzuia sandaku, sababu ng'ombe aliyekuwa amebeba sanduku aliyumba.
10Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza, na Yahweh akamua kwasababu Uza alishika na mkono wake sanduku. Akafa pale mbele za Mungu.
11Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza. Hiyo sehemu inaitwa Perezi Uza hadi leo.
12Daudi alimuogopa Mungu hiyo siku. Akasema, “Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?”
13Kwaiyo Daudi hakuleta sanduku kwenye mji wa Daudi, lakini aliweka pembeni mwa nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
14Sanduku la Mungu lilibaki nyumbani mwa Obedi Edomu kwa miezi mitatu. Kwaiyo Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.