Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mwanzo

Mwanzo 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
2Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.
3Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.
4Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.
5Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.
6Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.
8Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.
9Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
11Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.
12Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
14Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.
15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.
16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
17Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
18Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.

19Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake.
20Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.
21Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.
22Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.
23Henoko aliishi miaka 365.
24Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
25Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.
26Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
27Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
28Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.”
30Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake.
31Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.
32Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.