Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mwanzo

Mwanzo 23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sara akaishi mika mia moja na ishirini na saba. Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara.
2Sara akafa katika Kiriathi Arba, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abraham akaomboleza na kumlilia Sara.
3Kisha Abraham akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa, akanena na watoto wa kiume wa Hethi, akisema,
4“Mimi ni mgeni kati yenu. Tafadhari nipatieni mahali pa kuzikia miongoni mwenu, ili kwamba niweze kuzika wafu wangu.”
5Wana wa Hethi wakamjibu Abraham, wakasema,
6“Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako.”
7Abraham akainuka na kusujudu chini kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi.
8Akawaambia, akisema, “ikiwa mmekubali mimi kuzika wafu wangu, ndipo nisikilizeni, msihini Efroni mwana wa Sohari kwa ajili yangu.
9Mwambieni aniuzie pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake. Kwa bei kamili aniuzie waziwazi mbele ya watu kama miliki ya kuzikia.”
10Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi, hivyo Efroni Mhiti akamjibu Abraham alipowasikia wana wa Hethi, wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake, akasema,
11“Hapana, bwana wangu, nisikilize. Ninakupatia shamba na pango ambalo limo ndani yake. Ninakupatia mbele ya wana wa watu wangu. Ninakupatia uzike wafu wako.”
12Kisha Abraham akasujudu chini mbele ya watu wa nchi ile.
13Akamwambia Efroni watu wa nchi ile wakisikiliza, akasema, ikiwa uko radhi, tafadhari nisikilize. Nitalipia shamba. Chukua fedha kwangu, na nitazika wafu wangu pale.”
14Efroni akamjibu Abraham, akisema,
15“Tafadhari bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kinathamani ya shekeli mia nne za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? wazike wafu wako.”
16Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Helthi wakisikiliza, shekeli mia nne za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.
17Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa
18kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake.

19Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani.
20Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.