Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Nahumu

Nahumu 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yule ambaye atakuharibu vipande vipande anakuja dhidi yako. Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu.
2Maana Yehova anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa wateka nyara waliwaharibu na kuharibu matawi ya zabibu zao.
3Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, na watu hodari wamevaa nguo nyekundu; magari ya vita yameandaliwa yanang'ara kwenye vyuma vyake wakati wa mchana, na mikuki ya mivinje inarushwa hewani.
4Magari ya vita yapo kasi kwenye mitaa; yanakimbia mbele na nyuma katika mitaa. Yapo kama kurunzi, na yanakimbia kama radi.
5Yule ambaye atakuvunja vipande vipande anawaita maafisa wake; wanajikwaa kila mmoja kwa mwingine katika kutembea kwao; wanaharakisha kuushambulia ukuta wa mji. Ngao kubwa imetayarishwa kujikinga na hawa washambuliaji.
6Malango kwenye mito yamelazishwa kufunguka, na jumba la mfalme linaanguka kwenye uharibifu.
7Husabu amevuliwa mavazi yake na amachukuliwa; watumishi wake wa kike wanaomboleza kama njiwa, wanavipiga vifua vyao.
8Ninawi ni kama bwawa la maji linalovuja, watu wake kwa pamoja wanakimbia kama maji yanayotiririka. Wengine wanasema, “Simama, simama,” lakini hakuna anayegeuka nyuma.
9Chukua nyara ya fedha, kuchua nyara ya dhahabu, maana hakuna mwisho wake, kwa fahari ya vitu vyote vizuri vya Ninawi.
10Ninawi ipo tupu na imeharibiwa. Moyo wa kila mtu unayeyuka, magoti ya kila mmoja yanagongana pamoja, na uchungu upo kwa kila mmoja; sura zao wote zimepauka.
11Sasa liko wapi pango la simba, sehemu ambapo simba wadogo hula chakula, sehemu ambapo simba dume na simba jike walitembea, pamoja wana-simba, ambapo hawakuogopa kitu chochote?
12Simba alirarua mawindo yake vipande vipande kwa ajili ya watoto wake; aliwanyonga mawindo wake kwa ajili ya wake zake, na kulijaza pango lake mawindo, makao yake kwa mizoga iliyoraruliwa.
13“Tazama, mimi nipo kinyume na wewe- hili ni neno la Yehova wa majeshi. Nitayachoma magari yenu ya vita katika moshi, na upanga utateketeza simba wenu vijana. Nitazuia nyara zenu kutoka kwenye nchi yangu, na sauti za wajumbe wenu hazitasikika tena.”