Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 8

Mithali 8:20-35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Ninazalisha kilicho bora kuliko fedha safi. Natembea katika njia ya haki,
21katika mapito ambayo huelekea kwenye haki, ili niwape urithi wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao.
22Yehova aliniumba tokea mwanzo- mwazoni mwa matendo yake ya nyakati za kale.
23Tokea enzi za kale niliwekwa katika nafasi- tokea kwanza, tokea mwanzo wa dunia.
24Kabla ya bahari, mimi nilizaliwa- kabla ya kuwepo chemchemi zenye maji tele.
25Kabla ya milima na vilima kuwekwa, mimi nilizaliwa.
26Nilizaliwa kabla ya Yehova hajaiumba dunia wala makonde, hata mavumbi ya kwanza katika dunia.
27Nilikuwepo alipoziimarisha mbingu, wakati alipochora mstari katika sura ya kilindi.
28Nilikuwepo alipoimarisha anga la juu na wakati wa kutengeneza kina cha chemchemi.
29Nilikuwepo alipotengeneza mipaka ya bahari, ili maji yasisambae kuvuka pale alipoyaamuru, na wakati anaamuru misingi ya dunia sehemu ya kukaa.
30Nilikuwa kando yake, kama fundistadi mkuu, na mimi nilikuwa furaha yake siku kwa siku, nikifurahi mbele zake daima.
31Nilikuwa nikifurahi katika dunia yake yote na furaha yangu ilikuwa kwa wana wa wanadamu.
32Na sasa, wanangu, nisikilizeni, maana wale wazishikao njia zangu watakuwa na furaha.
33Sikilizeni fundisho langu na mpate hekima; wala msilipuuze.
34Anisikilizaye atakuwa na furaha- kila siku akitazama katika malango yangu, akinisubiri pembeni mwa milango ya masikani yangu.
35Maana yeyote anionaye mimi, anapata uzima, naye atapata kibali kwa Yehova.

Read Mithali 8Mithali 8
Compare Mithali 8:20-35Mithali 8:20-35