Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 30

Mithali 30:7-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Vitu viwili ninakuomba, usivikatalie kwangu kabla sijafa:
8Majivuno na uongo viweke mbali nami. Usinipe umasikini wala utajiri, nipe tu chakula ninachohitaji.
9Maana nikipata vingi zaidi, nitakukana wewe na kusema, “Yehova ni nani?” Au kama nitakuwa masikini, nitaiba na kukufuru jina la Mungu wangu.
10Usimkashifu mtumwa mbele ya bwana wake, au atakulaani na utapata hatia.
11Kizazi ambacho kinachomlaa baba yao na hakimbariki mama yao,
12kizazi hicho ni safi katika macho yao wenyewe, lakini hawajaoshwa uchafu wao.
13Hicho ni kizazi- jinsi gani macho yao yanakiburi na kope zao zimeinuka juu! -
14kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na mifupa ya taya zao ni visu, ili waweze kumrarua masikini wamtoe duniani na mhitaji atoke miongoni mwa wanadamu.
15Ruba anamabinti wawili, “Toa na Toa” wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisememi, “Inatosha”:
16Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, “Inatosha.”

Read Mithali 30Mithali 30
Compare Mithali 30:7-16Mithali 30:7-16