Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 29

Mithali 29:5-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.
6Mtu mbaya hunaswa kwenye mtego wa dhambi yake mwenyewe, bali yeye atendaye haki huimba na kufurahi.
7Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.
8Mwenye dhihaka huutia moto mji, bali wale wenye busara huigeuza ghadhabu.
9Mtu mwenye busara anapojadiliana na mpumbavu, hughadhabika na kucheka, hakutakuwa na utulivu.
10Mkatili humchukia mwenye ukamilifu na hutafuta maisha ya mwenye haki.
11Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
12Kama matawala atazinagatia uongo, maafisa wake wote watakuwa waovu.
13Mtu masikini na mkandamizaji wanafanana, maana Yehova huyapa nuru macho yao wote.
14Kama mfalme atamhukumu masikini kwa uaminifu, kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.
15Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.
16Watu waovu wanapotawala, uovu huongezeka, bali wenye kutenda haki wataona anguko la watu waovu.

Read Mithali 29Mithali 29
Compare Mithali 29:5-16Mithali 29:5-16