Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 29

Mithali 29:20-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
20Je unamwona mtu mwenye haraka katika maneno yake? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
21Mwenye kumdekeza mtumwa wake tangu ujana, mwisho wake itakuwa taabu.
22Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi na bwana mwenye hasira sana hutenda dhambi nyingi.
23Kiburi cha mtu humshusha chini, bali mwenye roho ya unyenyekevu atapewa heshima.
24Anayeshirikiana na mwizi huyachukia maisha yake mwenyewe; husikia laana na wala hasemi chochote.
25Kumwogopa binadamu ni mtego, bali mwenye kumtumaini Yehova atalindwa.
26Wengi huutafuta uso wa mtawala, bali kutoka kwa Yehova huja haki kwa ajili yake.
27Mtu dhalimu ni chukizo kwa wenye kutenda haki, bali mwenye njia ya haki ni chukizo kwa watu waovu.

Read Mithali 29Mithali 29
Compare Mithali 29:20-27Mithali 29:20-27