Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 25

Mithali 25:3-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Kama mbingu ni kwa kimo na dunia ni kwa kina, ndivyo hivyo moyo wa wafalme hauchunguziki.
4Ondoa takataka kutoka kwenye fedha na mfua vyuma anaweza kutumia fedha katika ufundi wake.
5Pamoja na hayo, waondoe watu waovu mbele ya mfalme na kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa kutenda haki.
6Usijitukuze mwenyewe mbele ya mfalme na usisimame katika sehemu iliyoteuliwa kwa watu wakuu.
7Ni bora yeye akuambie, “Njoo hapa” kuliko wewe kujiaibisha mbele ya mkuu.
8Usiharakishe kufanya kuhukumu, kwa kile ulichokishuhudia. Maana utafanya nini mwishoni, wakati jirani yako atakapokuaibisha?
9Jitetee kesi yako kati ya jirani yako na wewe na usifunue siri ya mtu mwingine,
10au vinginevyo anayekusikia ataleta aibu juu yako na taarifa mbaya juu yako haiwezi kunyamazishwa.
11Kunena maneno yenye kuchaguliwa vizuri, ni kama nakshi za dhahabu iliyoungwa kwenye fedha.
12Kama pete ya dhahabu au kito kilichotengenezwa kwa dhahabu safi ndivyo lilivyo karipio la busara kwenye sikio linalosikia.
13Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wenye kumtuma; huyahifadhi maisha ya mabwana wake.
14Kama mawingu na upepo bila mvua ndivyo alivyo mwenye kujisifu kuhusu zawadi asiyoitoa.
15Kwa uvumilivu mtawala anaweza kushawishiwa na ulimi raini unaweza kuvunja mfupa.
16Kama utapata asali, kula ya kutosha- vingenevyo, ukila nyingi sana, utaitapika.
17Usiweke mguu wako kwenye nyumba ya jirani yako mara nyingi, anaweza kuchoshwa nawe na kukuchukia.
18Mtu anayetoa ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake ni kama rungu lililotumiwa katika vita, au upanga, au mshale mkali.
19Kumtumaini mtu asiye mwaminifu wakati wa taabu ni kama jino bovu au mguu unaoteleza.
20Kama mtu anayevua nguo katika hali ya baridi, au kama siki iliyotiwa kwenye magadi, ndivyo alivyo anayeimba wimbo kwa mwenye moyo mzito.
21Kama adui yako ana njaa, mpe chakula ale na kama ana kiu, mpe maji ya kunywa,
22maana utamwekea mkaa juu ya kichwa chake na Yehova atakupa thawabu.
23Ni hakika upepo wa kaskazini huleta mvua, ndivyo mtu anayesema siri hufanya sura zikasirike.
24Ni bora kuishi kwenye pembe ya darini kuliko kuchangia nyumba pamoja na mwanamke mgomvi.
25Kama maji ya baridi kwa mwenye kiu, ndivyo ilivyo habari njema kutoka nchi ya mbali.
26Kama chemchemi iliyochafuliwa au kisima kilichoharibiwa ndivyo alivyo mtu mwema ambaye huyumbayumba mbele ya watu waovu.
27Si vema kula asali nyingi mno; hivyo ni kama kutafuta heshima baada heshima.

Read Mithali 25Mithali 25
Compare Mithali 25:3-27Mithali 25:3-27