Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 22

Mithali 22:18-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
18maana itakuwa furaha kwako kama utayaweka ndani yako, kama yote yatakuwa katika midomo yako.
19Basi tumaini lako liwe kwa Yehova, ninayafundisha kwako leo- hata kwako.
20Sijakuandikia wewe misemo thelathini ya mafundisho na maarifa,
21kwa kukufundisha kweli katika maneno haya yenye uaminifu, ili uwe na majibu yenye kutegemewa kwa waliokutuma?
22Usimwibie masikini kwa sababu ni masikini, au kumponda kwenye lango,
23maana Yehova ataitetea kesi yao, na atawaibia uzima wale waliowaibia masikini.
24Usifanye urafiki na mtu mwenye kutawaliwa na hasira na wala usiambatane pamoja na mwenye hasira kali,
25au utajifunza njia zake na utakuwa chambo kwa nafsi yako.
26Usiwe miongoni mwao wapigao mikono, mwenye kuahidi madeni.
27Kama umekosa njia za kulipa, nini kitaweza kuzuia mtu kuchukua kitanda chako chini yako?
28Usiondoe jiwe la mpaka la wahenga ambalo baba zako wameweka.

Read Mithali 22Mithali 22
Compare Mithali 22:18-28Mithali 22:18-28