Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 22

Mithali 22:1-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Jina jema huchaguliwa dhidi ya utajiri mwingi na fadhila ni bora kuliko fedha na dhahabu.
2Watu matajiri na masikini wanafanana katika hili - Yehova ni muumba wao wote.
3Mtu mwenye hekima huiona taabu na kujificha mwenyewe, bali mjinga huendelea mbele na huumia kwa ajili yake.
4Thawabu ya unyenyekevu na kumcha Yehova ni utajiri, heshima na uzima.
5Miiba na mitego hulala katika njia ya wakaidi; yeye anayelinda maisha yake atakuwa mbali navyo.
6Mfundishe mtoto njia inayompasa na wakati akiwa mzee hatayaacha mafundisho hayo.
7Watu matajiri huwatawala watu masikini na mwenye kukopa ni mtumwa wa yule anayekopesha.
8Yule anayepanda udhalimu atavuna taabu na fimbo ya hasira yake itanyauka.
9Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa, maana anashiriki mkate wake pamoja na masikini.
10Mfukuze mbali mwenye dhihaka, na ugomvi utaondoka, mashindano na matukano yatakoma.
11Anayependa moyo safi na mwenye maneno ya neema, atakuwa rafiki yake mfalme.
12Macho ya Yehova huyaangalia maarifa, bali huyapindua maneno ya wadanganyifu.
13Mtu mvivu husema, “Kuna simba mtaani! Nitauwawa sehemu za njia.”
14Kinywa cha malaya ni shimo lenye kina kirefu; hasira ya Yehova huchochewa dhidi ya yule anayetumbukia ndani yake.
15Upumbavu umefungwa katika moyo wa mtoto, lakini marudi ya fimbo huutoa.
16Anayewanyanyasa watu masikini ili kuongeza mali yake, au kuwapa matajiri, atakuwa masikini.
17Tega sikio lako na usikilize maneno ya wenye busara na utumia moyo wako katika maarifa yangu,
18maana itakuwa furaha kwako kama utayaweka ndani yako, kama yote yatakuwa katika midomo yako.
19Basi tumaini lako liwe kwa Yehova, ninayafundisha kwako leo- hata kwako.
20Sijakuandikia wewe misemo thelathini ya mafundisho na maarifa,
21kwa kukufundisha kweli katika maneno haya yenye uaminifu, ili uwe na majibu yenye kutegemewa kwa waliokutuma?
22Usimwibie masikini kwa sababu ni masikini, au kumponda kwenye lango,
23maana Yehova ataitetea kesi yao, na atawaibia uzima wale waliowaibia masikini.
24Usifanye urafiki na mtu mwenye kutawaliwa na hasira na wala usiambatane pamoja na mwenye hasira kali,

Read Mithali 22Mithali 22
Compare Mithali 22:1-24Mithali 22:1-24