Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 1

Mithali 1:19-31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Ndivyo zilivyo njia za kila ambaye hupata utajiri kwa udhalimu; mapato ya udhalimu huondoa uhai wa wenye utajiri.
20Hekima inalia kwa sauti mtaani, inapaza sauti katika viwanja;
21katika mitaa inalia kwa sauti kuu, kwenye maingilio ya milango ya mji inasema
22“Mpaka lini enyi wajinga mtapenda kuwa wajinga? Mpaka lini enyi wenye dhihaka mtapenda dhihaka, na hadi lini enyi wapumbavu, mtachukia maarifa?
23Zingatia karipio langu; nitatoa mawazo yangu kwa ajili yenu; nitawafahamisha maneno yangu.
24Nimeita, nanyi mkakataa kusikiliza; nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyezingatia.
25Lakini mumedharau mafundisho yangu yote na wala hamkuzingatia maelekezo yangu.
26Nitacheka katika taabu yenu, nitawadhihaki wakati wa kupatwa taabu-
27hofu ya kutisha itawapata kama tufani na maafa yatawakumba kama upepo wa kisulisuli, taabu na uchungu vitawapata.
28Halafu wataniita, nami sitawajibu; wataniita katika hali ya kukata tamaa lakini hawataniona.
29Kwa sababu wamechukia maarifa na hawakuchagua kuwa na hofu ya Yehova,
30hawakufuata mafundisho yangu na wakayadharau masahihisho yangu yote.
31Watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa kwa matunda ya hila zao wenyewe.

Read Mithali 1Mithali 1
Compare Mithali 1:19-31Mithali 1:19-31