Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 17

Mithali 17:12-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Ni bora kukutana na dubu aliyeporwa watoto wake kuliko kukutana na mpumbavu katika upumbavu wake.
13Mtu anaporudisha mabaya badala ya mema, mabaya hayatatoka katika nyumba yake.
14Mwanzo wa mafarakano ni kama mtu anayefungulia maji kila mahali, hivyo ondoka kwenye mabishano kabla ya kutokea.
15Yeye ambaye huwaachilia watu waovu au kuwalaumu wale wanaotenda haki - watu hawa wote ni chukizo kwa Yehova.
16Kwa nini mpumbavu alipe fedha kwa kujifunza hekima, wakati hana uwezo wa kujifunza?
17Rafiki hupenda kwa nyakati zote na ndugu amezaliwa kwa ajili ya nyakati za taabu.
18Mtu asiyekuwa na akili hufanya ahadi zenye mashariti na kuanza kuwajibika kwa madeni ya jirani yake.
19Apendaye mafarakano anapenda dhambi; ambaye hutengeneza kizingiti kirefu sana kwenye mlango wake husababisha kuvunjia kwa mifupa.
20Mtu mwenye moyo wa udanganyifu hapati chochote ambacho ni chema; na mwenye ulimi wa ukaidi huanguka kwenye janga.
21Mzazi wa mpumbavu huleta majonzi kwake mwenyewe; baba wa mpumbavu hana furaha.
22Moyo mchangamfu ni dawa njema, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
23Mtu mwovu hukubali rushwa ya siri ili kupotosha njia za haki.
24Mwenye ufahamu huelekeza uso wake kwenye hekima, bali macho ya mpumbavu huelekea ncha za dunia.
25Mwana mpumbavu ni huzuni kwa baba yake na uchungu kwa mwanamke aliyemzaa.
26Pia, si vizuri kumwadhibu mwenye kutenda haki; wala si vema kuwachapa mjeledi watu waadilifu wenye ukamilifu.
27Mwenye maarifa hutumia maneno machache na mwenye ufahamu ni mtulivu.

Read Mithali 17Mithali 17
Compare Mithali 17:12-27Mithali 17:12-27