3Kabidhi kwa Yehova kazi zako zote na mipango yako itafanikiwa.
4Yehova alifanya kila kitu kwa kusudi lake, hata waovu kwa ajili ya siku ya taabu.
5Yehova anamchukia kila mtu mwenye moyo wa majivuno, ingawa wanasimama imara, hawakosi kupata adhabu.
6Kwa agano la uaminifu na udhamini uovu husafishwa na kwa kumcha Yehova watu hujitenga na ubaya.
7Njia za mtu zinapompendeza Yehova, huwafanya hata adui zake huyo mtu wawe na amani naye.
8Bora kitu kidogo pamoja na haki, kuliko mapato makubwa pamoja na udhalimu.
9Katika moyo wake mtu hunuia njia yake, bali Yehova huziongoza hatua zake.