Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 16

Mithali 16:16-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
16Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu. Kuchagua kupata ufahamu ni zaidi kuliko fedha.
17Njia kuu ya watu waadilifu hujitenga na ubaya; mwenye kuyahifadhi maisha yake huilinda njia yake.
18Kiburi hutangulia kabla ya uharibifu na moyo wa kujivuna kabla ya maangamizi.
19Ni bora kunyenyekea miongoni mwa watu masikini kuliko kugawana ngawira pamoja watu wenye kiburi.
20Mwenye kutafakari yaliyofundishwa hupata kilicho chema na wenye kumtumaini Yehova watafurahi.
21Mwenye hekima moyoni anaitwa ufuhamu na utamu wa hotuba huongeza uwezo wa kufundisha.
22Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake ambaye nayo, bali adhabu ya wapumbavu ni upumbavu wao.
23Moyo wa mtu mwenye hekima hutoa busara katika kinywa chake na huongeza ushawishi katika midomo yake.
24Maneno yenye kufaa ni sega la asali -matamu kwenye nafsi na huponya mifupa.
25Kuna njia ambayo huonekana sawa kwa mtu, bali mwisho wake ni njia ya mauti.
26Hamu ya kibarua humfanyia kazi; njaa yake humsihi kuendelea.
27Mtu duni huchimba madhara na usemi wake ni kama moto unaounguza.
28Mtu mkaidi huchochea mafarakano na umbeya huwafarakanisha marafiki.
29Mtu wa vurugu humdanganya jirani yake na kumwongoza kwenye mapito ambayo si mema.

Read Mithali 16Mithali 16
Compare Mithali 16:16-29Mithali 16:16-29