Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 14

Mithali 14:19-34

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Hao ambao ni waovu watainama mbele yao walio wema na wale wenye uovu watasujudu kwenye malango ya wenye haki.
20Mtu masikini huchukiwa hata na marafiki zake, bali watu matajiri wanamarafiki wengi.
21Yeye ambaye huonyesha dharau kwa jirani yake anafanya dhambi, bali yule ambaye huonyesha fadhila kwa masikini anafuraha.
22Je wale wanaofanya njama mbaya hawapotei? Bali wale wenye mpango wa kutenda mema watapokea agano la uaminifu na udhamini
23Katika kazi zote ngumu huja faida, bali palipo na maongezi tu, huelekea kwenye umasikini.
24Taji ya watu wenye busara ni utajiri wao, bali upuuzi wa wapumbavu huwaletea upuu zaidi.
25Shahidi mkweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo hupumua uongo.
26Mtu anapokuwa na hofu ya Yehova, pia anakuwa na matumaini zaidi ndani yake; vitu hivi vitakuwa kama sehemu imara ya ulinzi kwa watoto wa mtu huyu.
27Kumcha Yehova ni chemchemi ya uzima, ili kwamba mtu aweze kujiepusha kutoka katika mitego ya mauti.
28Utukufu wa mfalme upo katika idadi kubwa ya watu wake, bali pasipo watu mfalme huangamia.
29Mtu mvumilivu anaufahamu mkubwa, bali mtu mwepesi wa kuhamaki hukuza upuuzi.
30Moyo wenye raha ni uzima wa mwili, bali husuda huozesha mifupa.
31Anayemkandamiza masikini humlaani Muumba wake, bali anayeonyesha fadhila kwa wahitaji humtukuza yeye.
32Mtu mwovu huangushwa chini kwa matendo yake mabaya, bali mtu mwenye haki anakimbilio hata katika kifo.
33Hekima hukaa katika moyo wa ufahamu, bali hata miongoni mwa wapumbavu hujiachilia mwenyewe kwa kujulikana
34Kutenda haki huliinua taifa, bali dhambi ni chukizo kwa watu wowote.

Read Mithali 14Mithali 14
Compare Mithali 14:19-34Mithali 14:19-34