Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 14

Mithali 14:1-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Mwanamke mwenye busara huijenga nyumba yake, bali mwanamke mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
2Yeye aendaye kwa uaminifu humcha Yehova, bali mkaidi humdharau katika njia zake.
3Katika kinywa cha mpumbavu hutoka chipukizi la kiburi chake, bali midomo ya wenye busara itawalinda.
4Pale pasipo na mifugo hori la kulishia ni safi, bali mazao mengi huweza kupatikana kwa nguvu za maksai.
5Shahidi mwaminifu hasemi uongo, bali shahidi wa uongo hupumua uongo.
6Mwenye dharau hutafuta hekima na hakuna hata, bali maarifa huja kwa urahisi kwa mwenye ufahamu.
7Nenda mbali kutoka kwa mtu mpumbavu, maana hutapata maarifa kwenye midomo yake.
8Hekima ya mtu mwenye busara ni kuifahamu njia yake mwenyewe, bali upuuzi wa wapumbavu ni udanganyifu.
9Wapumbavu hudharau wakati sadaka ya hatia inapotolewa, bali miongoni mwao waaminifu hushiriki fadhila.
10Moyo unayajua machungu yake mwenyewe na hakuna mgeni anayeshiriki furaha yake.
11Nyumba ya waovu itaangamizwa, bali hema ya watu waaminifu itasitawi.
12Kuna njia ambayo huonekana sawa kwa mtu, lakini mwisho wake huelekea mauti tu.
13Moyo unaweza kucheka lakini bado ukawa katika maumivu na furaha inaweza kukoma ikawa huzuni.
14Yule asiyemwaminifu atapata anachostahili kwa njia zake, bali mtu mwema atapata kilicho chake.

Read Mithali 14Mithali 14
Compare Mithali 14:1-14Mithali 14:1-14